Kesi ya Rais
wa zamani wa Marekani itaanza wiki ya pili ya Februari katika Bunge la Seneti,
baada ya kuwasilishwa mashitaka katika taasisi hiyo mapema wiki ijayo, maafisa
wa chama cha Democratic katika Baraza la Congress wamesema.
“Mara baada
ya faili hizo kutayarishwa, kesi itaanza wiki ya Februari 8,” amesema Chuck
Schumer, kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, ambapo Donald
Trump atasikilizwa kwa madai ya “kuchochea uasi”.
Chuck
Schumer hapo awali alikuwa amewaambia wenzake kwamba mashtaka “yatapelekwa
katika Bunge la Seneti Jumatatu”.
Kufikia
sasa, Joe Biden amejizuia kuingilia kati suala hili, akibaini kwamba ni kwa
Bunge la Seneti lenyewe kuweka masharti ya kesi ya mtangulizi wake.
Donald Trump anatuhumiwa kuwa aliwahimiza wafuasi wake kuanzisha shambulio katika majengo ya Bunge la Seneti, Capitol Hill, Januari 6, wakati wawakilishi wabunge na maseneti walikuwa wakiidhinisha ushindi wa Joe Biden aliyetangazwa kushinda uchaguzi wa urais.
EmoticonEmoticon