Kim jong-un Akiri Kwamba Mpango Wa Kiuchumi Wa Korea Kaskazini Umefeli

 

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amekubalia kuwa mpango wake wa kiuchumi wa miaka mitano kwa nchi hiyo ambayo imejitenga, ulishindwa kufikia malengo yaliyowekwa "katika karibu kila sekta".

Alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha dharura cha chama chake cha Workers' Party kikao ambacho ni cha nane katika historia ya nchi hiyo.

Korea Kaskazini ilifunga mipake yake Januari mwaka jana kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona licha ya madai kwamba hakujawahi kuwa na maambukizi ya virusi hivyo nchini humo.

Hatua hiyo imesababisha kujitenga na majirani zake ambayo pia ni washirika wake wa karibu China.


EmoticonEmoticon