Kimbunga Eloise Chasababisha Mafuriko Mabaya Katika Mji Wa Beira Msumbiji

 

Baadhi ya maeneo ya kati ya taifa la Msumbiji yamekumbwa na mafuriko baada ya kimbunga Eloise kupiga eneo lililo karibu na mji wa Beira na upepo wenye kasi ya kilomita 160 kwa saa .

Beira ilipokea milimita 250 za mvua katika kipindi cha saa 24 , kulingana na Taasisi ya kitaifa ya hali ya hewa nchuni humo INAM.

Baadhi ya maafisa na mashirika ya misaada yanachunguza kiwango cha uharibifu huo ili kuweza kuwasaidia walioathirika, na kujaribu kurudisha umeme na mawasiliano ambayo yalikatwa katika baadhi ya maeneo. Watu wameuawa kulingana na maafisa.

Kimbunga hicho hatahivyo kimeshushwa hadhi na kutajwa kuwa dhoruba ya kitropiki na kilitabiriwa kuelekea Zimbabwe na kaskazini mwa Afrika Kusini mataifa ambayo tayari yamekumbwa na mvua kubwa.


EmoticonEmoticon