Kinyang'anyiro
katika jimbo la Georgia kinachotarajiwa kuamua nani atakuwa na udhibiti wa
bunge la Seneti kinaendelea kuwa na ushindani mkali huku vituo vya kupiga kura
vikiwa vimefungwa.
Kituo cha habari cha CBS News mshirika wa BBC kimesema vyama
vyote viwili vinakaribiana mno. Matokeo yanatarajiwa kuanza kutangazwa saa
kadhaa tokea sasa lakini ikiwa matokeo yataendelea kuonesha ukaribu wa namna
hiyo huenda matokeo ya mwisho yakachukua muda kutangazwa.
Rais mteuliwa Joe Biden wa chama cha Democrats anahitaji
kushinda uchaguzi huu ili aweze kupata udhibiti wa mabunge yote mawili.
Wakati huohuo, rais wa chama cha Republican anayeondoka
madarakani Donald Trump anahitaji kushinda kiti kimoja tu ili adhibiti bunge
hilo la Seneti.
Wabunge wa
Republican Kelly Loeffler na David Perdue sasa hivi ndio wanaoshikilia viti
hivyo viwili. Bi. Loeffler anakabiliana na Reverend Raphael Warnock huku Bwana
Perdue akipambana na aliyekuwa mwanahabari Jon Ossoff.
Hakuna kati ya wagombea hao ambaye alipata asilimia 50 ya kura zilizopigwa kama inavyohitajika kuibuka na ushindi wa moja kwa moja katika uchaguzi uliofanyika Novemba hatua iliyolazimisha kufanyika kwa duru ya pili kulingana na sheria za uchaguzi za jimbo la Georgia.
EmoticonEmoticon