Kiongozi Mkuu wa Iran Akataa Chanjo Ya Corona Nchini Humo

 

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema ni marufuku kwa Nchi yake kupokea chanjo ya Corona kutoka Marekani na Ulaya, huku akisema kama kutakuwa na ulazima wataagiza chanjo kutoka Mataifa mengine.

“Marekani na Nchi za Ulaya hasa Uingereza hawaaminiki kabisa, wanaweza kuleta chanjo kumbe ndio zikawa zinaeneza maambukizi zaidi” - Ayatollah

“Hata Ufaransa hatutaki chanjo zao miaka ya 1980 na 1990 waliwahi kuwa na skendo ya kusambaza damu yenye virusi vya UKIMWI” - Ayatollah


EmoticonEmoticon