Kiongozi Wa Upinzani Wa Urusi Akamatwa Baada Ya Kuwasili Nyumbani

 

Mkosaji wa rais wa Urusi Vradimir Putin , Alexei Navalny amekamatwa baada ya kurejea mjini Moscow kwa ndege akitokea Ujerumani, miezi mitano baada ya kushambuliwa kwa sumu ya neva ambayo nusura imuue.

Mwanaharakati huyo, mwenye umri wa miaka 44, alichukuliwa na polisi katika kitengo cha udhibiti wa paspoti katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo.

Maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika katika viwanja tofauti vya ndege vya mjini Moscow kuipokea ndege yake iliyokuwa ikijtokea mjini Berlin, lakini ndege yake ilielekezwa kwenye uwanja tofauti.

Bw Navalny anazilaumu mamlaka za Urusi kwa jaribio la kumuua mwaka jana. Utawa la Kremlin unakana kuhusika na shambulio hilo la sumu.

Madai ya mwanasiasa huyo wa upinzani hata hivyo yamekua yakiungwa mkono na ripoti za waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi.

Kukamatwa kwa Bw Navalny kumelaaniwa na Muungano wa Ulaya, Ufaransa na Italia , ambao wametoa wito aachiliwe mara moja.

Mshauri ajaye wa masuala ya usalama wa taifa wa Rais mteule wa Marekani Joe Biden ipia ameunga mkono wito huo "Shambulio la Kremlin dhidi ya Bw Mr Navalny si ukiukaji tu wa haki za binadamu, lakini pia ni unyanyasaji kwa watu wa Urusi ambao wanataka sauti yao isikike ," Jake Sullivan alisema.


EmoticonEmoticon