Wabunge wa
Democratic wanataka kesi isikilizwe haraka wakati Rais Joe Biden anaanza muhula
wake wakisema kusomewa mashtaka kamili kwa Trump ni muhimu kabla ya nchi na
Congress kusonga mbele
Kiongozi wa Wa-Republican katika baraza la seneti Mitch
McConnell anapendekeza kuchelewesha kuanza kwa kesi ya mashtaka dhidi ya Rais
wa zamani Marekani, Donald Trump kwa wiki moja au zaidi ili kumpa muda Trump wa
kutathmini kesi hiyo.
Wabunge wa Democratic ambao walipiga kura ya kumfungulia
mashtaka Trump wiki iliyopita kwa kuchochea vurugu kwenye jengo la Bunge hapo
Januari 6 wanaashiria kwamba wanataka kesi isikilizwe haraka wakati Rais Joe
Biden anaanza muhula wake wakisema kusomewa mashtaka kamili kwa Trump ni muhimu
kabla ya nchi na Congress kusonga mbele.
Lakini McConnell aliwaambia maseneta wenzake wa GOP kwenye simu kwamba ucheleweshaji mfupi utampa muda Trump wa kutathmini kesi hiyo na kusimama na timu yake ya wanasheria inayohakikisha mchakato unaofaa.
EmoticonEmoticon