Taarifa
kutoka nchini Somali zasema kuwa kituo cha redio cha wanamgambo wa Alshabab cha
Al-Andalus kimevamiwa kwa shambulio la anga jana usiku katika wilaya ya
Kuntuwarey eneo la Shabelle.
Kulingana na tovuti za wanaounga mkono wanamgambo hao,
shambulio hilo limesababisha watu watatu kujeruhiwa katika nyumba iliyo mkabala
na jengo la kituo hicho cha redio ambalo limeharibika vibaya.
Inaaminika kuwa shambulio hilo la anga limetekelezwa kwa
kutumia ndege isiyokuwa na rubani.
Hadi kufikia sasa mkuu wa jeshi la Marekani barani Afrika
hajasema lolote kuhusiana na shambulio hilo ingawa nchi hiyo imetekeleza
mashambulizi kadhaa nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni.
Aidha serikali ya Somali pia nayo haijasema lolote juu ya shambulio hilo lililotokea eneo la Kuntuwarey.
EmoticonEmoticon