Kocha Wa Real Madrid Apatikana Na Corona

 

Kocha wa Real Madrid ya Hispania Raia wa Ufaransa Zinedine Zidane ametangazwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona na sasa atatakiwa kujitenga kwa muda ili kuepuka kuwa chanzo cha kueneza Corona kwa wengine.

Taarifa za Zidane kupata maambukizi zinakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka club yake iondolewe katika michuano ya Copa del Rey kwa kufungwa na Alcoyano, kipigo ambacho kimeleta maswali juu ya hatma yake Bernabeu.


EmoticonEmoticon