Kremlin Yapuuza Miito Ya Kumwachia Navalny

Ikulu ya Urusi, Kremlin, imepuuza matakwa ya mataifa ya magharibi ya kumuachia huru mwanasiasa wa juu wa upinzani Alexei Navalny na kukosoa miito yake ya kufanyika maandamano makubwa ya umma. 

Msemaji wa rais Vladmir Putin, Dmitry Peskov amesema serikali mjini Moscow haiwezi na haitayazingatia matamko yanayotolewa na mataifa ya magharibi kwa sababu hilo ni suala la ndani. 

Navalny alikamatwa mara baada ya kuwasili kutoka nchini Ujerumani alikopelekwa kwa matibabu Agosti mwaka uliopita kufuatia kisa cha kupewa sumu ya kuharibu mfumo wa Neva. 

Kukamatwa kwake kumekosolewa vikali na mataifa ya magharibi, huku Markekani, Umoja wa Ulaya, Ufaransa na Canada zikitoa wito wa kuachiwa kwake. 

Washirika wa Navalny wamewataka Warusi kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuandamana hadi hadi ikulu ya Kremlin, baada ya mwanasiasa huyo kuhukumiwa kifungo cha siku 30.


EmoticonEmoticon