Kwa Mara Ya Kwanza Messi Apigwa Kadi Nyekundu

 

Lionel Messi alionyeshwa kadi nyekundu ya kwanza katika ya maisha yake ya soka akiwa na FC Barcelona katika Mchezo waliopoteza dhidi ya Athletic Bilbao katika fainali ya Kombe la Super Cup la Uhispania iliyopigwa usiku wa kuamkia leo

FT' FC Barcelona 2-3 Athletic Bilbao

Messi,alimuumiza Asier Villalibre katika dakika za mwisho za muda wa ziada, Mwamuzi Gil Manzano alikosa tukio hilo mwanzoni lakini baada ya ukaguzi wa VAR, alimwonyesha Messi kadi nyekundu moja kwa moja,

Hii inakuwa kadi ya kwanza nyekundu ambayo Messi amewahi kupokea kama mchezaji wa Barcelona, ​​akiwa katika mechi yake ya 753 katika kilabu hiyo.


EmoticonEmoticon