Lady Gaga, Jenifer Lopez Kutumbuiza Kwenye Hafla Ya Uapisho Wa Joe Biden

 

Mastaa wa muziki kutoka Nchini Marekani Lady Gaga na Jennifer Lopez ni miongoni mwa watu mashuhuri waliowekwa kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa rais mteule wa Marekani Bwana Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris siku ya Jumatano (Januari 20,2021).


Lady Gaga ataimba wimbo wa Taifa wakati rais mteule na makamu wa rais mteule, Kamala Harris, wakiapishwa siku hiyo na Lopez anatarajiwa kutoa onyesho la muziki.

Bwana Joe Biden (78), ataapishwa rasmi januari 20, na kuwa Rais wa 46 wa Marekani baada ya kuthibitishwa kama mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 3, 2020 nchini humo.


EmoticonEmoticon