Mahakama Nchini Uganda Yaamuru Jeshi, Polisi Kuondoka Nyumbani Kwa Bobi Wine

 

Mahakama nchini Uganda imeliamuru jeshi na polisi kuondoka nyumbani kwa Bobi Wine

Bobi Wine hajaondoka nyumbani kwake tangu wakati wa uchaguzi siku 11 zilizopita, uliomtangaza kuwa mshindi wa pili baada ya Yoweri Museveni.

Hukumu ya mahakama Kuu siku ya Jumatatu imekuja baada ya suala hilo kufikishwa mahakamani na mawakili wa Bobi Wine.

Serikali ilidai kuwa ilihiaji kumzuia kupanga maandamano. Bobi Wine alidai kuwa mchakato wa kura ulikumbwa na udanganyifu.

Katika hatua nyingine, Tume ya uchaguzi nchini Uganda imekana taarifa kuwa ilichapisha kwenye tovuti yake matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye tovuti yake kisha kuliondoa chapisho hilo.

Tume hiyo tarehe 17 mwezi Januari ilimtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi kwa 59% ya kura zilizopigwa. Mgombea wa nafasi hiyo Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, 35%. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo bado hayajachapishwa, tume ilisema siku ya Jumapili.

Lakini imezifanyia majaribio anuani ambazo matokeo yatachapishwa. Anuani za tovuti zilizojaribiwa ziliondoshwa, ilisema tume hiyo.

''Si kweli kuwa Tume ya Uchaguzi Uganda imefuta au kuondoa matokeo kwani matokeo rasmi hayajachapishwa. ''Matokeo yatachapishwa kwenye magazeti na tovuti,'' iliandika kwenye ukurasa wa Twitter.


EmoticonEmoticon