Malawi
imepata pigo kubwa baada ya mawaziri wake wawili kufariki dunia kutokana na
Covid 19.
Waziri wa habari wa Malawi, Gospel
Kazako amethibitisha kuwa mawaziri hao ambao ni Waziri wa serikali za mitaa,
Lingson Belekanyama na Waziri wa uchukuzi Sidik Mia wamefariki ndani ya masaa
mawili tofauti.
Mwishoni mwa juma, rais wa nchi hiyo Lazarus Chakwera alitoa hotuba maalumu kwa njia ya radio kwa taifa akitoa wito wa kuheshimiwa kwa hatua zilizowekwa za kupambana na maambukizi ya Covid 19 kufuatia ongezeko kubwa katika vifo na maambukizi ya virusi hivyo.
Bw Chakwera anatarajiwa kutoa hotuba nyingine kwa taifa baadae leo, kwa mujibu wa Kazako.
EmoticonEmoticon