Marekani Yakasirishwa Na Uamuzi Wa Mahakama Kuu Ya Pakistan

 

Mahakama kuu ya Pakistan imemwachia huru Ahmed Saeed Omar Sheikh aliyehukumiwa hapo awali baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mauaji ya mwandishi wa habari wa Marekani Daniel Pearl mnamo mwaka 2002. 

Msemaji wa ikulu ya Jen Psaki amesema Marekani imekasirishwa na uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Pakistan na amesisitiza kuwa Psaki amesema Marekani haikufurahishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Pakistan wa kumwachia huru Sheikh na watuhumiwa wengine watatu waliohusika na utekaji nyara na mauaji ya kinyama ya Daniel Pearl na kwamba hiyo ni dharau kwa wahanga wa ugaidi kila mahala ulimwenguni na ndani ya Pakistan. 

Msemaji huyo wa ikulu ya Marekani ameitaka serikali ya Pakistan kuangalia upya vipengee katika sheria zake pamoja na kuiruhusu Marekani imfungulie mashtaka Omar Sheikh kwa mauaji ya kinyama ya raia wa Marekani na mwandishi wa habari.

Mahakama Kuu ya Pakistan iliamuru kuachiwa huru kwa Mpakistani Ahmed Saeed Omar Sheikh mwenye uraia wa Uingereza pia ilitupilia mbali rufaa ya kupinga kuachiwa kwake iliyowasilishwa na familia ya Pearl pamoja na serikali ya Pakistan.


EmoticonEmoticon