Marekani Yataka Wasafiri Wanaoingia Wawekwe Karantini

 

Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza mpango wake wa kupambana na janga la COVID-19. 

Hapo jana aliyatia saini maagizo kadhaa ya kiutendaji yenye lengo la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. 

Miongoni mwa masharti yanayotokana na maagizo hayo ni kuwataka wasafiri wote wanaoingia kwa ndege nchini Marekani kuthibitisha kwamba wamechukuliwa vipimo vya COVID-19, na kuwekwa karantini baada ya kuwasili. 

Masuala mengine yanayopewa kipaumbele katika maagizo hayo ya rais Biden ni kuongeza utengenezaji wa chanjo na idadi ya vituo vya kuwapima watu, kama msingi wa kufunguliwa tena kwa shule na shughuli za biashara. 

Hata hivyo, bado hakuna maelezo ya kina juu ya kilichomo katika maagizo hayo. Rais Biden amesema utawala wa mtangulizi wake, Donald Trump ulishindwa kupambana na janga la virusi vya corona.


EmoticonEmoticon