Merkel Aelekeza Lawama Kwa Trump Kufuatia Uvamizi Wa Majengo Ya Bunge Marekani

 

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ameelekeza lawama kwa rais wa marekani Donald Trump kufuatia vurugu za wafuasi wa rais huyo walivamia majengo ya bunge.

Akizungumza akiwa mjini Berlin, Merkel amesema matukio ya jana katika majengo ya bunge ya Capitol Hill mjini Washington yalimghadhabisha.Merkel ameongeza kwamba anasikitishwa mno kwamba hadi sasa Trump hajakubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba.

Merkel pia alielezea matumaini kuhusu rais mteule Joe Biden atakayechukua usukani Januari 20 kudumisha demokrasia.

Maafisa wa Urusi pia wamezungumzia vurugu za jana mjini Washington wakisema ni ushahidi kuwa Marekani inadidimia, huku mwengine akisema demokrasia ya Marekani inajikongoja kwenye miguu yote miwili.

Viongozi wengi ulimwenguni wameshutumu uvamizi huo wa jana unaodaiwa ulichochewa na Trump.


EmoticonEmoticon