Rais wa
Mexico Andres Manuel Lopez Obrador, amesema kwamba utawala wa Joe Biden
unastahili kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro wa wahamiaji kutoka Mexico
wanaishi Marekani.
Obrador
amesema kwamba amekuwa akipendekeza kwamba raia wa Mexico ambao wamekuwa
wakifanya kazi nchini Marekani kwa mda mrefu wanastahili kupewa vibali na
kutambuliwa kulingana na sheria.
Amesema
kwamba hatua kama hiyo inastahili kusaidia mipango iliyopo ya kusaidia mataifa
masknini ya Amerika ya kati na kusini mwa Mexico, ambayo raia wake wengi
wanaingia Marekani kila mwaka kama wakimbizi.
Lopez Obrador ametaka utawala wa Joe Biden kufanya mabadiliko makubwa kwa sera za uhamiaji na amesema kwamba ana matumaini makubwa kwamba rais mpya wa Marekani atasdhughulikia swala hilo kwa haraka sana.
EmoticonEmoticon