Misri, Sudan Na Ethiopia Zakosa Kuafikiana Kuhusu Mzozo Wa Bwawa

 

Misri, Sudan na Ethiopia, zimetangaza jana Jumapili kwamba zimeshindwa kufikia makubaliano katika mazungumzo, yaliyosimamiwa na Umoja wa Afrika kusuluhisha mvutano kuhusu bwawa kubwa la Ethiopia la mradi wa umeme kwenye mto wa Blue Nile. 

Mawaziri wa nchi za nje pamoja na wa unyunyizaji maji wa nchi hizo, walikutana kwa mara ya pili ndani ya wiki moja kwa njia ya video katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa jinsi ya kurejea kwenye mazungumzo yao juu ya kujazwa maji pamoja na operesheni ya bwawa hilo kubwa. 

Wizara ya mambo ya nje ya Misri imesema nchi yake na Ethiopia zilipinga pendekezo la Sudan. Nayo wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema Sudan ilikataa pendekezo la Afrika Kusini la pande zote husika kukutana tofauti na wataalamu wa Umoja wa Afrika. 

Mnamo Novemba, Sudan ilisusia mazungumzo yaliyoitishwa na Afrika Kusini ambayo ndiyo mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.


EmoticonEmoticon