Msafara wa
wahamiaji kutoka Amerika Kusini uliokuwa ukielekea nchini Marekani umekutana na
marungu na gesi za kutoa machozi nchini Guatemala, ambapo vikosi vya usalma
vilifunga njia yao ya kupita kuelekea Marekani.
Maelfu ya watu walizuiwa kwenye barabara karibu na mpaka wa
Guatemala na Honduras. Serikali imesema haingekubali "matembezi ya umati
wa watu kinyume cha sheria ".
Wahamiaji wanaokadiriwa kuwa 7,000 , wengi wao kutoka
Honduras, wameingia katika siku za hivi karibuni, wakikimbia umasikini na
ghasia.
Wanatumaini kusafiri hadi Mexico, na baadaye kuufikia mpaka
wa Marekani.
Kila mwaka,
maelfu ya wahamiaji wa Amerika ya kati hujaribu safari hii ili kujaribu kufika
Marekani, mara nyingi hutemea kwa miguu.
Rais mteule wa Marekani Joe Biden, kutoka chama cha Democrat,
ameapa kuondoa sera kali za uhamiaji zilizowekwa na mtangulizi wake, Donald
Trump, kutoka Republican.
Lakini utawala wa Bw Biden ,ambao utachukua mamlaka Jumatano, umewaonya wahamiaji kutofanya safari , kwa sababu sera za uhamiaji hazitabadilishwa mara haraka.
EmoticonEmoticon