Msamaha Wa Donald Trump Wawafikia Lil Wayne Na Kodak Black

 

Rais Donald Trump ametoa msamaha kwa watu zaidi ya 100 wakiwemo rapa Lil Wayne na rapa Kodak Black katika siku yake ya mwisho ofisini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Kayleigh McEnany usiku wa kuamkia leo.

Lil Wayne alikuwa akikabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 gerezani baada ya kukiri kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria wakati wa akisafiri kwa ndege binafsi mnamo Desemba 2019.

Kodak Black, ambaye jina lake halisi ni Bill Kapri, alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka mitatu gerezani Novemba 2019 kwa kosa la kughushi Nyaraka ili kupata silaha

Hafla ya kuapishwa Joe Biden itafanyika leo Mchana kwa saa za Marekani huku ikihudhuriwa na idadi ndogo tu ya watu kutokana na janga la COVID-19,

Mapema hii leo imefanyika ibada maalum kuwakumbuka maelfu ya watu waliofariki dunia baada ya kuugua Corona nchini Marekani.

Biden na Makamu wake Kamala Harris wanaapishwa rasmi Leo Jumatano (Januari 20), Biden anakuwa Rais wa 46 wa Marekani Baada ya kuibuka Mshindi wa Uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba mwaka jana.


EmoticonEmoticon