Mtandao Wa YouTube Waizuia Chanel Ya Raisi Wa Marekani Donald Trump

 

Mtandao wa Youtube umeingia katika orodha ya mitandao ya kijamii ambayo imeamua kumuadhibu Rais Donald Trump baada ya kile kinachodaiwa kuhamasisha vurugu za kupinga matokeo halali yaliyompa ushindi Joe Biden katika uchaguzi mkuu wa Marekani.

Taarifa kutoka uongozi wa Youtube zinaeleza kuwa, akaunti ya Trump imezuiliwa kwa muda wa wiki moja na inawezekana ikawa zaidi ya hapo baada ya kuchapisha maudhui yanayoenda kinyume na muongozo wa watumiaji wa mtandao huo kwa kuhamasisha vurugu.

Hivi karibuni, mtandao wa Twitter uliifuta moja kwa moja akaunti ya Rais huyo na kusema kuwa kuiacha akaunti hiyo kutahatarisha usalama wa Marekani, hali iliyomfanya Rais huyo kutumia ukurasa rasmi wa Ikulu kutupa lawama kwa mtandao huo na kuahidi kufungua mtandao wake.


EmoticonEmoticon