Muda wa Kuondoka Vikosi Vya Kigeni Nchini Libya Wamalizika

 

Muda wa mwisho wa kuondoka kwa vikosi vya kigeni kutoka nchini Libya ulimalizika mnamo siku ya Jumamosi lakini hakukuwepo na dalili yoyote kwamba askari hao walikuwa wanajiandaa kuondoka. 

Mnamo Oktoba 23, pande hasimu nchini Libya zilifikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye mazungumzo yaliyofanyika mjini Geneva, Uswisi. 

Makubaliano hayo yalijumuisha tarehe ya mwisho ndani ya miezi mitatu ya kuondolewa vikosi vya askari wa kigeni na mamluki.

Libya imekuwa katika machafuko tangu alipopinduliwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011 na imegeuka kuwa uwanja wa mapambano kati ya makundi yanayopingana ambayo yanaungwa mkono na nchi za kigeni. 

Uturuki inaiunga mkono Serikali ya mjini Tripoli inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa na imewapeleka wanajeshi na vifaa vya vita kuisaidia serikali hiyo kupambana na majeshi hasimu yaliyoko mashariki mwa Libya na yanayoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar anayeungwa mkono na Urusi, Misri na Umoja wa nchi za Kiarabu.


EmoticonEmoticon