Mwanamke Mweusi Ambaye Raisi Biden Anataka Kumuweka Kwenye Noti Ya Marekani

 

Utawala wa Joe Biden unasema utaona namna wataavyoweza kuharakisha kupitisha muswada wa kutaka dola 20 ya Marekani kuwa na sura ya Harriet Tubman baada ya utawala wa Trump kuchelewesha zoezi hilo baada ya utawala wa Barack Obama kuanzisha mswada huo.

"Idara ya fedha watachukua hatua ya kuanza tena jitihada za kumuweka bi. Harriet Tubman katika noti ya dola $20 ,"Jen Psaki amesema kutoka idara ya habari ya Ikulu ya Marekani.

"Wanataka kusema fedha zetu, zinaashiria historia yetu na utofauti wetu , na picha ya Harriet Tubman ikiwekwa kwenye noti mpya ya dola 20 itaweza kuleta taswira ya namna hiyo."

Utawala wa Obama ilitangaza mwaka 2016 kuwa wataenda kumuweka Bi.Harriet Tubman katika fedha hiyo ya $20 na kumuondoa Andrew Jackson.

Lakini utawala wa Trump ulisema mwaka 2019 kuwa mabadiliko hayo yatachelewa na yanaweza kufanyika labda mwaka 2028 kwasababu za changamoto za kiteknolojia.

Na sasa Jen Psaki anasema wataongez kasi ili zoezi hilo lifanyike haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya CNN inasema msemaji mmoja wa idara ya fedha anasema wanasubiri tu kupata uthibitisho wa kufanya hivyo.

Kama mabadiliko haya yakifanyika , Harriet Tubman atakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa katika fedha ya Marekani.


EmoticonEmoticon