Mwanaume
aliyekuwa na hofu kubwa ya kusafiri kwa ndege kutokana na janga la virusi vya
corona aliishi bila kugundulika katika eneo salama katika uwanja wa kimataifa
wa Chicago' kwa miezi mitatu, wamesema waendesha mashitaka nchini Marekani.
Aditya Singh, mwenye umri wa miaka 36, alikamatwa Jumapili
baada ya mfanyakazi mmoja wa ndege kumtaka atoe kitambulisho chake.
Alimuonesha kitambulisho cha kazi (badge) ambayo inadaiwa
kuwa kilikuwa ni cha meneja mmoja katika uwanja huo ambaye aliripotiwa kuwa
kitambulisho chake kilipote.
Polisi wanasema Bw Singh aliwasili kutoka Los Angeles na
kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa O'Hare tarehe 19 Oktoba mwaja
jana.
Anaripotiwa
kupatikana na kitambulisho cha muhudumu (badge) katika uwanja wa ndege na
alikuwa "anaogopa kwenda nyumbani kwasababu ya Covid", alisema naibu
Mwanasheria mkuu wa jimbo Kathleen Hagerty, katika jarida la Chicago Trubune.
Aliweza kuishi kwa msaada aliopewa na wasafiri wengine,
alimwambia hakimu katika kesi dhidi yake.
Jaji wa kaunti Susana Ortiz alieleza kushangwazwa sana na
tukio hilo.
"Kwa hiyo, kama ninakuelewa vizuri, ni kwamba unaniambia
kuwa mtu ambaye haruhusiwi, ambaye sio muajiriwa anadaiwa kuishi katika eneo salama
la uwanja wa ndege wa kimataifa wa O'Hare kuanzia tarehe 19 Oktoba, 2020 hadi
tarehe 16 Januari 2021, na hakugundulika?
Ninataka kukuelewa kwa usahihi," alimwambia mwendesha mashitaka ambaye alikuwa akiainisha mashitaka Jumapili.
EmoticonEmoticon