Rais wa
Ghana Akufo-Addo, ameapishwa kama rais kwa mhula wa pili madarakani, siku moja
baada ya kutokea vurugu bungeni.
Akufi – Addo
alimshinda mpinzania wake rais wa zamani John Mahama katika uchaguzi
uliofanyika mwezi Desemba na ambao ulikuwa na ushindani mkali sana.
Wabunge wa
Ghana, ambao walichaguliwa hivi karibuni walipigana bungeni baada ya kukosa
kukubaliana namna ya kumteua spika.
Uchaguzi wa
spika ulikuwa umepangwa kufanyika kwa njia ya siri, lakini wabunge kutoka chama
kinachotawala cha New Patriotic NPP, walikuwa wakionyesha hadharani
waliyempigia kura, jambo ambalo liliwakera wabunge wa upinzani.
Wakati mmoja,
mbunge wa chama kinachotawala alichukua karatasi za kupigia kura kwa lazima
wakati uchaguzi ulikuwa unaendelea na hivyo kuzua mgogoro.
Polisi wenye
silaha na wanajeshi wameitwa bungeni katika juhudi za kurejesha utulivu.
Chama
kinachotawala na upande wa upinzani, wana idadi sawa ya wabunge. Kuna mbunge
mmoja asiyekuwa na chama cha kisiasa.
Mahakama
ilimzuia mmoja wa wabunge wa upinzani kushiriki katika kura hio ya kujaza
nafasi ya spika, baada ya kesi kuwasilishwa mahakamani kupinga ushindi wake
katika uchaguzi mkuu. Mbunge huyo hata hivyo alikubaliwa na bunge kushiriki
uchaguzi huo.
Wanasiasa wa upinzani wamedai kuwepo udanganyifu katika uchaguzi wa mwezi Desemba na wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu kabisa kutaka uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali.
EmoticonEmoticon