Rwanda,Burundi
na Umoja wa falme za kiarabu zimeongezwa kwenye orodha ya nchi zilizowekewa
marufuku ya kuingia nchini Uingereza.
Rwanda na Burundi zinajiunga na Tanzania, Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Afrika Kusini ambazo pia zimewekewa marufuku hiyo na
Uingereza.
Hatua hiyo inalenga kudhibiti kuenea kwa aina mpya ya kirusi
cha Afrika Kusini, na marufuku hiyo inaanza kufanya kazi siku ya Ijumaa saa
saba kwa saa za Uingereza
Raia wa Uingereza, Ireland na raia wenye haki ya makazi
nchini Uingereza wataruhusiwa kuingia lakini kwa sharti la kujitenga kwa siku
10 wakiwa nyumbani.
Watu wenye
ushawishi kwenye mitandao ya kijamii walitembelea Dubai majuma ya hivi karibun
,pamoja na kuwepo marufuku ya kusafiri iwapo hakuna ulazima wa kusafiri.
Walisisitiza kuwa safari zao ni kwa ajili ya kazi, lakini
idara ya usafiri imesem misamaha yoyote ya kusafiri ambayo kawaida ipo
haitakuwepo, ikiwemo kusafiri kwa sababu za kibiashara.
Pia safari za moja kwa moja za ndege za abiria kutoka
Uingereza kwenda Umoja wa falme za kiarabu zitapigwa marufuku.
Kwa nyongeza ya nchi hizo inamaanisha kuwa nchi 33 zimewekewa marufuku hiyo mpaka sasa.
EmoticonEmoticon