Nchi Nyingi Zaanza Kuchukua Tahadhari Baada Ya Maambukizi Ya Corona Kuongezeka

 

Maambukizi ya virusi vya corona yanazidi kuongezeka kote duniani sawia na wale wanaokufa kutokana na virusi hivyo, jambo lililopelekea nchi kadhaa duniani kutangaza vikwazo vipya mwishoni mwa wiki. 

Zimbabwe mwishoni mwa wiki ilitangaza kufunga nchi mara moja, nayo Gibralter ikachukua hatua sawa na hiyo, huku Ugiriki ikaongeza muda wa vikwazo vyake hadi Januari 10. 

Gavana wa mji wa Tokyo huko Japan ametaka hali ya dharura itangazwe huku Ufaransa ikitangaza marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri.

Kwengineko Ulaya, Ujerumani inatarajiwa kuongeza muda wake wa hatua za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona kupita Januari 10, muda uliokuwa umewekwa awali kutokana na ongezeko la maambukizi. 

Kulingana na wanasiasa nchini humu hospitali na wahudumu wa afya wanalemewa na mzigo wa wagonjwa. Kansela Angela Merkel na viongozi wa majimbo wanatarajiwa kukubaliana kuongeza vikwazo watakapokutana Jumanne. Bado haijawekwa wazi vikwazo hivyo vitaongezwa kwa muda gani.


EmoticonEmoticon