Mlimbwende
wa Marekani Kim Kardashian na mume wake msanii Kanye West wamekuwa wakipata
ushauri wa ndoa yao,lakini mtandao wa TMZ nchini humo umegundua kwamba kwa
suala la wawili hao kutengana limekuwepo kwa muda mrefu lakini hawajakata
tamaa.
Vyanzo
kadhaa vilivyo na habari zinazowahusu wawili hao vimeambia mtandao huo nchini
Marekani , kwamba ndoa hiyo ilikuwa katika matatizo makubwakatika nusu ya
mwisho wa mwaka 2020.
Habari zinasema kwamba Kim alikuwa tayarikuomba talakakatika tukio moja lakini kwasababu Kanye alikuwa anakumbwa na tatizo la kiakili akaona kwamba sio vyema kuchukua hatua hiyo wakati ambapo hali ya mume wake sio nzuri.
EmoticonEmoticon