Staa wa muziki wa Rap kutoka Nchini
Marekani Nicki Minaj amekutwa na hatia ya
kukiuka hakimiliki ya nyota wa R&B, Tracy Chapman.
Mwaka 2018 Chapman alimshtaki Nicki Minaj akisema ameiga
sehemu ya wimbo wake wa 'Baby Can I Hold You Tonight' katika wimbo wake wa
'Sorry' aliomshirikisha Nas,
Chapman amekubali kesi hiyo kufika mwisho baada ya kukubali kulipwa na Nicki Minaj dolla 450,000 (Takribani Bilioni 1 za Kitanzania) ambazo zinajumuisha gharama za Chapman na zile za kulipia kesi hadi kufikia sasa ili kesi hiyo iishe.
EmoticonEmoticon