Papa Abadili Sheria Ya Kanisa Majukumu Zaidi Kwa Wanawake

 

Katika hatua nyingine ya kuelekea usawa zaidi kwa wanawake kwenye Kanisa Katoliki, Papa Francis hii leo amebadilisha rasmi sheria za kanisa hilo kuwaruhusu kusoma neno la Mungu, kuhudumu katika altare na kusaidia kugawa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. 

Uamuzi huo uliotolewa kupitia amri ya papa, unarasimisha kile ambacho kimekuwa kikifanyika katika mataifa mengi yalioendelea kwa miaka kadhaa. 

Lakini kwa kuanzisha mabadiliko katika kanuni ya sheria za kanisa, itakuwa haiwezekani kwa maaskofu wahafidhina kuwazuwia wanawake katika majimbo yao kufanya majukumu hayo. 

Lakini Vatican imesisitiza kuwa majukumu haya ni tofauti na yale yanayofanywa na wanaojiandaa kwa ajili ya daraja takatifu la upadri.


EmoticonEmoticon