Papa Francis Asema Kukwepa chanjo ya Covid-19 ni mauaji ya kujitakia

 

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameiita hatua ya watu kukwepa kupata chanjo ya Covid-19 ni mauaji ya kujitakia akisema wale wanaokataa chanjo hiyo wanacheza na afya zao na pia maisha ya watu wengine. 

Kiongozi huyo mkuu wa kidini kwa upande mwingine amethibitisha kwamba binafsi atapata chanjo hiyo mwanzoni mwa wiki ijayo huku akiwaita watu wanaopinga chanjo hiyo kuwa wenye kupingana na kifo. 

Akizungumza na shirika la habari la Italia ametoa mwito kwa watu kujitokeza kupata chanjo hiyo akisema kwamba anaamini kimaadili kila mmoja anapaswa kupata chanjo.


EmoticonEmoticon