Raia wa
Uganda hii leo wanapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wapya wa bunge.
Akizungumza siku ya Jumatano
mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo jaji Simon Byabakama aliserma kwamba
wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni tisa huku wenzao wa jiniai ya kike
wakiwa zaidi ya milioni tisa.
Katika uchaguzi huo rais Yoweri
Museveni ambaye anatetea wadhfa wake anakabilia na upinzani mkali kutoka kwa
mwanamuziki wa zamani maarufu Bobi Wine.
Bobi Wine ni mgombea ambaye amevutia
idadai kubwa ya vijana nchini humo.
Rais Museveni anagombea muhula wa
sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Hatahhivyo rais Museveni anajivunia
utawala wake wa muda mrefu ambapo amefanya baadhi ya maenedeleo.
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.
EmoticonEmoticon