Rais Wa Malawi Anaanza Siku 21 Za Kufunga Na Maombi Kusitisha Corona Nchini Humo

 

Chakwera alisema ongezeko la maambukizi ni kubwa Malawi kwa sababu watu wengi akiwemo yeye mwenyewe walipuuzia masharti ya wataalam wa afya ya kujikinga na COVID-19 ikiwemo kuvaa barakoa

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera anasema amehuzunishwa na takwimu zinazoonesha ongezeko la karibuni la maambukizi ya virusi vya Corona nchini mwake. 

Katika hotuba ya Jumapili kwa njia ya redio alitangaza anaanza siku 21 za kufunga na kumuomba mungu aepushe janga ambalo limeongezeka tena. Wataalamu wa afya wanasema hali iliyopo nchini humo inahitaji zaidi ya maombi ya sala.

Malawi hivi karibuni imeshuhudia ongezeko katika kesi za virusi vya Corona. Tangu Alhamis nchi hiyo imekuwa ikithibitisha kesi nyingi za COVID kuwahi kurekodiwa.


EmoticonEmoticon