Rais mpya wa Marekani Joe Biden amesaini maagizo
ya kiutendaji yanayobatilisha mengine yaliyoewekwa na mtangulizi wake, Donald
Trump, yakiwemo yanayohusu mazingira, uhamiaji na mapambano dhidi ya COVID-19.
Kwa kuyasaini maagizo hayo Rais Biden amedhamiria kuonesha mabadiliko ya
mwelekeo wa siasa za Marekani, Mshauri wake wa magonjwa ya mlipuko, Dr. Anthony
Fauci ameuhutubia kwa njia ya video mkutano wa WHO, na kusema Marekani inarudi
tena kushirikiana na wengine Duniani kwa ajili ya chanjo kwa wote.
D. Fauci ameahidi kuwa Marekani itarejea tena WHO kama
Mwanachama>>”Marekani itabakia kuwa Mwanachama wa WHO, jana Rais Joe
Biden alisaini barua inayofuta tangazo la kujiondoa WHO na barua tayari
imetumwa kwa Katibu Mkuu wa UN na kwa Boss wa WHO Dr. Tedros”
Tedros, mwaka jana alikosolewa vikali na Donald Trump, kabla ya kuiondoa
Marekani WHO akiwatuhumu kushindwa kupambana na Corona, Dr Fauci pia amesema
Marekani inarejesha ufadhili wa kifedha WHO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon