Raisi Mteule Joe Biden Apewa Chanjo Ya Pili

 

Rais Mteule wa Marekani Joe Biden amepewa chanjo ya Corona kwa mara ya pili ambapo amesema akishaapishwa January 20,2021 na kuingia Ikulu, chanjo ya Corona itakuwa ni kipaumbele chake cha kwanza.

Marekani inaongoza kwa maambukizi ya Corona Duniani ikiwa na vifo 375,000 hadi sasa, na takribani Watu 3000 wanakufa kila siku.

Dozi Mil 25.5 zimesambazwa kwenye Hospitali na Zahanati mbalimbali Marekani lakini ni Watu Mil 9 pekee wamepewa chanjo hadi sasa.


EmoticonEmoticon