Raisi Wa Marekani Amuonya Raisi Wa Urusi Kuhusu Kuingilia Uchaguzi Wa Marekani

 

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi katika mawasiliano yao ya kwanza kwa njia ya simu, White House imeeleza.

Mazungumzo hayo ni pamoja na majadiliano kuhusu maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini Urusi na kuongezwa kwa mkataba wa silaha za nyuklia wa Marekani na Urusi

Bwana Putin alimpongeza rais mpya wa Marekani kwa kushinda uchaguzi,kwa mujibu wa taarifa ya Urusi.

Pande zote mbili zilisema zilikubaliana kudumisha mahusiano.

Rais wa zamani Barack Obama - ambaye chini yake Bwana Biden aliwahi kuwa Makamu wa Rais - pia alikosolewa kwa kushindwa kuchunguza Kremlin ilivyokuwa ikidhibiti Crimea, ilivamia Mashariki mwa Ukraine na kuingia Syria. 

White House na Kremlin zimesema nini kuhusu mazungumzo yao?

''Rais Biden aliweka wazi kuwa Marekani itasimama kidete kutetea maslahi ya taifa lake kwa vitendo vya Urusi vinavyotuathiri sisi au washirikawetu,'' ilisema taarifa ya Marekani.

Ikulu ya Marekani imesema marais hao waliozungumza kwa simu siku ya Jumanne pia walijadili kuhusu mashambulizi ya mtandaoni ya kampuni ya SolarWinds, ambayo kwayo Moscow ilinyooshewa kidole, ripoti zikieleza kuwa Kremlin iliwafadhili wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, na sumu ya mwanaharakati wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny.

Maafisa wa urusi wamesema Bw. Putin ''ameona kuwa kuweka sawa mahusiano kati ya Urusi na Marekani kutafanya kufikiwa kwa malengo na kulinda maslahi ya nchi zote mbili-ukizingatia jukumu walilonalo la kulinda usalama na uimara duniani.

"Kwa ujumla, mazungumzo kati ya viongozi wa Urusi na Marekani yalikuwa ya biashara na ya asili ya kweli," taarifa ya Kremlin iliongeza.

Viongozi hao wawili walionekana kutia saini makubaliano ya kurejesha New Start, makubaliano ya wakati wa Obama ambayo yanapunguza viwango vya silaha, makombora na virusha makombora miongoni mwa silaha za nyuklia za Marekani na Urusi.

Ulipaswa kumalizika mwezi ujao, na Bw Trump alikuwa amekataa kusaini.


EmoticonEmoticon