Rais wa Marekani Joe Biden leo anatarajiwa
kutangaza marufuku ambayo itawazuia kuingia Marekani Raia ambao sio Wamarekani
kutoka Uingereza, Ireland, Brazil na Mataifa mengi ya Ulaya.
Biden pia ataongeza muda wa zuio kwa Watu ambao wamesafiri
kwenda Nchini Afrika Kusini siku za karibuni nao hawatorushiwa kuingia Marekani.
Kirusi Kipya cha Corona kilichobainika Afrika ya Kusini
kimeonesha kuwa ni hatari zaidi kuliko virusi vilivyo katika Nchi nyingine
Duniani na kimeonekana kuathiri zaidi wagonjwa wengi nchini Afrika ya Kusini na
husambaa kwa haraka zaidi kuliko hata kile kirusi kipya kinachopatikana
Uingereza.
Kutokana na Kuwepo kwa kirusi hicho Afrika ya Kusini, Nchi
nyingi zimezuia safari za ndege kuingia na kutoka Nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon