Mahakama ya juu ya Korea Kusini leo
imethibitisha adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa Rais wa zamani wa Nchi
hiyo Park Geun Hye(68).
Mahakama hiyo imesema inakataa rufaa iliyowasilishwa na
Waendesha mashitaka dhidi ya muda uliopunguzwa wa adhabu ya kifungo gerezani
iliyotolewa Julai 2020.
Park anashitakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya
madaraka pamoja na hongo katika mashitaka mengine kwenye kashfa ya mwaka 2017
iliyosababisha kuondolewa madarakani.
Park ambaye ni Binti wa Dikteta wa kijeshi Park Chung Hee,
aliondolewa madarakani kufuatia wiki kadhaa za maandamano yaliyomtaka ajiuzulu,
Kiongozi huyo mara zote amekana mashitaka dhidi yake akisema anaandamwa kisiasa.
EmoticonEmoticon