Rapa Dr. Dre
bado yupo ICU akiwa chini ya uangalizi mkubwa wa Madaktari ikiwa wiki moja
baada ya kuugua ugonjwa wa aneurysm ya ubongo.
Vyanzo vya karibu na Rapa huyo mwenye umri wa miaka 55
vimeiambia TMZ kwamba madaktari wanaendelea
kufanya vipimo kadhaa ili kujua nini kilitokea na wamemtaka Dre kusalia ICU ili
kufuatilia kwa ukaribu zaidi hali yake
Katika
taarifa yake wiki iliyopita, Dre aliwaambia mashabiki kwamba "anaendelea
vizuri" na atatolewa hospitalini hivi karibuni. Alishukuru pia wafuasi
wake na Madaktari huko Cedars-Sinai
Dre alikimbizwa na gari la wagonjwa kutoka nyumba yake ya
Pacific Palisades hadi Kituo cha Matibabu cha Cedars-Sinai huko Los Angeles Jumatatu
iliyopita (Januari 4)
EmoticonEmoticon