Serikali ya
Rwanda imepiga marufuku usafiri wa umma na wa kibinafsi kati ya wilaya na mji
mkuu wa Kigali, baada ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Maafisa wa afya hata hivyo wamesema kwamba usafiri wa ndani
na nje ya nchi utaendelea lakini wasafiri wanahitajika kuwa na cheti kuonyesha
kwamba wamepimwa virusi vya Corona.
Watu 105 walifariki mwezi Desemba mwaka uliopita, na kuwa
mwezi ambao ulirekodi idadi kubwa zaidi ya vifo kutokana na virusi vya Corona
nchini Rwanda.
Maafisa wana Imani kwamba masharti ya kuzuia usafiri kati ya
wilaya yatasaidia kupunguza kiwango cha maambukizi.
Watu 820 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona na 30
kufariki kutokana na virusi hivyo nchini Rwanda
Msimamizi wa afya ya msingi nchini Rwanda Tharcisse Mpunga,
ameambia shirika la habari la serikali ya Rwanda kwamba kutokana na kiwango cha
maambukizi, Rwanda inastahili kusitisha shughuli za kawaida na watu
kulaazimishwa kukaa nyumbani na usafiri wa watu kuingia nchini humo kusitishwa
kwa mda wa siku 14 ili kudhibithi maambukizi.
Kulingana na masharti mapya, shughuli zote za biashara
zitatakiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni saa za Rwanda. Mikutano yote
imepigwa marufuku.
Kila mtu anatakiwa kuwa nyumbani kwake ifikapo saa nne usiku hadi saa kumi kamili asubuhi.
EmoticonEmoticon