Rwanda Yazifunga Shule Tena Kuzuia Maambukizi Ya Corona

 

Rwanda imetoa agizo la kufunga tena shule zote za umma kuanzia Januari 18, 2021 leo Jumatatu.

Wizara ya Elimu imesema kuwa shule zote za chekechea, msingi na za sekondari za umma na za kibinafsi zitafungwa katika mji wa Kigali kama njia moja ya kukabiliana na usambaaji wa virusi va corona hasa mjini Kigali.

Pia, wanafunzi wa shule za bweni watasalia katika shule zao na wataendelea kupokea huduma muhimu.

Wizara hiyo pia imeongeza kuwa shule zote nje ya mji wa Kigali zitaendelea kufunza na shughuli zingine za masomo kwa kuzingatia hatua kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 na pia muongozo huo utapitiwa tena katika kipindi cha wiki mbili zijazo kulingana na tathmini ya huduma ya afya.

Watu 22 walikufa kutokana na Covid19 kwa muda wa siku 7 zilizopita na kuifanya idadi ya waliokufa kutokana na corona hadi kuifikia sasa kuwa 142.

Haya yanajiri wakati bado ikitekelezwa marufuku ya siku 15 ya usafiri wa umma kati ya wilaya na mji mkuu Kigali ambapo pia biashara zote nchini humo husitishwa saa kumi na mbili jioni.


EmoticonEmoticon