Serikali Ya Ujerumani Yapendekeza Kurefusha Vizuizi Vya COVID-19

 

Serikali ya Ujerumani imependekeza leo kurefusha muda wa vizuizi vya sasa vya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona hadi katikati ya mwezi unaokuja, na kuchukua hatua ziada kupunguza viwango vya maambukizi ya aina mpya ya virusi hivyo. 

Hayo ni kulingana na shirika la habari la DPA ambalo limepata nakala ya waraka wa serikali kuelekea mkutano wa kansela Angela Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo utaofanyika baadae hivi leo. 

Hata hivyo duru zinazoshiriki majadiliano ya serikali zimearifu kuwa pendekezo hilo limekumbana na upinzani mkali hasa kutoka majimbo yanayoongozwa chama cha siasa za wastani za mrengo wa shoto cha SPD. 

Mawaziri wakuu wa majimbo hayo wanataka mapendekezo hayo yafanyiwe mabadiliko kadhaa huku kukiwa na mabishano juu ya iwapo vikwazo vikali zaidi vinahitajika. 

Serikali imependekeza kuimarisha kanuni za uvaaji barakoa kwenye usafiri wa umma na maduka pamoja na kuongeza shinikizo kwa waajiri kuwaruhusu watumishi kufanya kazi nyumbani.


EmoticonEmoticon