Shirika La Afya Duniani Lakataa Kulegeza Masharti

 

Shirika la Afya Duniani, WHO tawi la Ulaya limesema leo kuwa ni mapema mno kulegeza vizuizi vya kukabiliana na janga la corona barani Ulaya licha ya kupungua kwa visa vipya katika nchi nyingi. 

Hans Kluge, mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya amesema 30 kati ya nchi 53 za Ulaya zimeshuhudia kupungua pakubwa kwa visa hivyo katika kipindi cha siku 14. 

Kluge hata hivyo amesema viwango vya maambukizi kote Ulaya bado vipo juu mno, na kuathiri mifumo ya afya na utoaji huduma na kufanya iwe mapema mno kulegeza vizuizi. 


EmoticonEmoticon