Tahadhari Ya Moto Yasababisha Jengo La Capitol Kufungwa Kwa Muda

 

Jengo la bunge la Capitol mjini Washington DC lilifungwa kwa muda kufuatia tahadhari ya usalama siku mbili kabla ya rais mteule Joe Biden kuapishwa rasmi.

Maafisa wa polisi wanasema kwamba walichukua hatua hiyo kama tahadhari baada ya mashahidi kuripoti moshi uliokuwa ukifuka.

Moto huo ulikuwa umbali wa majumba kadhaa. Zoezi la kujiandaa kwa kuapishwa kwa Joe Biden lilifutiliwa mbali kwa muda.

Watu watano walifariki tarehe sita mwezi Januari wakati wafuasi wa Trump walipokuwa wakiandamana kuvamia jengo la Capitol ambalo ndio linashirikisha ukumbi wa bunge la Marekani.

Usalama umeimarishwa, huku maelfu ya walinzi wa kitaifa wakipelekwa katika eneo hilo na katikakati ya maeneo ya Washington DC.

Tahadhari iliosamabazwa mapema kwa wafanyakazi wa jengo hilo la Capitol ilisema kwamba ukumbi huo umefungwa huku watu wakizuiwa kuingia ama kutoka.

Lakini wazima moto wa Washington DC baadaye walisema kwamba waliitikia wito wa kukabiliana na moto uliokuwepo na kuuzima. Hakukuwa na tishio lolote kwa umma, maafisa walisema.


EmoticonEmoticon