Timu Ya Wataalamu Wa WHO Kuwasili China Alhamis

 

Wataalamu kutoka Shirika la Afya Duniani WHO, wanatarajiwa kuwaisili nchini China wiki hii, kuanza uchuguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu juu ya chimbuko la janga la virusi vya corona. 

Kamisheni ya afya ya China ilisema awali katika taarifa fupi kwamba watalaamu hao watawasili siku ya Alhamisi na kukutana na wenzao wa China. Baadae msemaji wa wizara ya mambo ya nje Zhao Lijian, alitoa tamko kamili na kusema kuwa baada ya majadiliano kati ya pande mbili. 

Serikali ya China iliidhinisha timu ya wataalamu wa WHO kuzuru China Janauri 14 ili kubadilishana mitazamo na wanasayansi wa China na wataalamu wa tiba juu ya ushirikiano wa kisayansi kuhusu kufuatilia chimbuko la virusi vya corona. 

Kumekuwepo na mzozo kuhusu ziara ya wataalamu hao na wiki iliyopita WHO ilitangaza kuwa China imewazuwia kuingia. Beijing ilijibu kwa kusema kuwa maandalizi yalikuwa bado yanafanyika.


EmoticonEmoticon