Wafuasi wa
rais Faustin Archange Touadera wanaendelea kusherehekea mjini Bangui kufuatia
ushindi wake wa asilimia 54 katika uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati.
Hata hivyo, kuna wasiwasi ya kutokea mapigano baada ya maelfu
ya watu kushindwa kupiga kura kutokana na hali mbaya ya uslama, waasi wakiwa
wanadhibithi sehemu kubwa ya nchi hiyo inayoorodheshwa kati ya nchi zenye
misukosuko mingi sana duniani.
Tume ya uchaguzi imesema kwamba matokeo hayo yana maana
kwamba hakuna duru ya pili ya uchaguzi itafanyika.
Aliyekuwa waziri mkuu Anicet George Pologuele, amemaliza
katika nafasi ya pili akiwa na asilimia 21 ya kura huku Martin Ziguele
akimaliza katika nafasi ya tatu na asilimia 7.
Kulikuwa na wagombea 16 wa urais wakiwemo wanawake watatu,
katika uchaguzi mkuu wa urais Jamhuri ya Afrika ya kati.
Wagombea wa upinzani wamesema kwamba kulikuwepo udanganyifu
mkubwa katika hesabu ya kura.
Uchaguzi huo ulifanyika licha ya mashambulizi ya muungano wa
makundi ya waasi, ambayo yalisababisha maelfu ya watu kukosa kupiga kura.
Serikali imemshutumu aliyekuwa rais wa nchi hiyo François
Bozizé, kwa kujaribu kufanya mapinduzi.
Bozize alizuiliwa kugombea urais.
Amekanusha madai kwamba anawaunga waasi kupindua serikali.
Waendesha mashtaka wameanzisha uchunguzi dhidi ya Bozize kuhusiana na madai ya kutaka kupindua serikali.
EmoticonEmoticon