Trump Aahidi Kwa Namna Fulani Lazima Tu Atarudi

 

Rais mstaafu Donald Trump aliyemaliza muda wake ameondoka mjini Washington, saa chache kabla ya kuapishwa kwa rais mpya Joe Biden.

Katika hotuba fupi kwa wafanyakazi, wafuasi na jamaa zake waliokusanyika katika uwanja wa ndege za kijeshi nje ya Washington, Trump alisema kuwa miaka minne iliyopita imekuwa ya aina yake. 

Kabla ya kupanda kwa mara ya mwisho ndege rasmi ya rais kuelekea jimboni Florida yalipo makaazi yake, Trump amesema ''kwa namna fulani atarudi tena". 

Aliongeza kuwa utawala wake umepata mafanikio makubwa, na kuwaahidi wafuasi wake kuwa ataendelea kuwapigania. 

Trump hakumtaja Biden kwa jina lakini alisema kuwa anautakia uongozi mpya kila la heri. 

Trump ni raisi wa kwanza katika muda wa zaidi ya miaka 150 kukosa kuhudhuria sheria ya kuapishwa kwa mrithi wake.


EmoticonEmoticon