Trump Aahidi Makabidhiano Ya Madaraka Kwa Amani

Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza makabidhiano ya madaraka kwa njia iliyonyooka ifikapo Januari 20, baada ya mabaraza ya bunge kuthibitisha ushindi wa rais mteule Joe BidenKupitia taarifa aliyotoa punde tu baada ya mchakato huo wa mabaraza ya Bunge kumalizika, Trump amesema hakubaliani kabisa na matokeo ya uchaguzi hata hivyo kutakuwa na mapokezano ya madaraka kwa njia ya amani.

Ameongeza kwamba japo hatua hiyo ni mwisho wa muhula wake wenye mafanikio makubwa katika historia ya urais nchini Marekani, ni mwanzo tu wa mapambano wa kuifanya Marekani kuwa imara tena.

Ameyasema hayo leo huku akiendelea na madai yake kwamba uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.

Taarifa hiyo ilitolewa kupitia ukurasa wa twitter wa mkurugenzi wake wa mitandao ya kijamii Dan Scavino kwa kuwa kurasa za Trump katika mitandao ya Twitter, Facebook na Instagram zimefungwa kwa muda kufuatia tukio la jana ambapo wafuasi wake walivamia majengo ya bunge mjini Washington.


EmoticonEmoticon