Utawala wa Trump umeirudisha Cuba katika orodha ya ‘nchi zinazofadhili ugaidi‘ na kuiwekea vikwazo vipya vinavyoweza kukwamisha ahadi ya Biden kufufua uhusiano na serikali ya kikomunisti katika nchi hiyo ya kisiwani.
Waziri wa nchi za nje wa Marekani
Mike Pompeo, ametangaza hatua hiyo jana Jumatatu akitaja ushirikiano kati ya
Cuba na waasi wa Colombia, ushirikiano wa Cuba na serikali ya siasa za mrengo
wa kati ya Venezuela pamoja na hatua ya Cuba kuwakaribisha wakimbizi wa
Marekani kuwa miongoni mwa sababu zilizowafanya kuchukua hatua hiyo.
Suala la kuitangaza Cuba kuwa taifa linalofadhili ugaidi limejadiliwa kwa miaka mingi na ni miongoni mwa hatua kadhaa za mwisho za sera ya nchi za nje ambazo utawala wa Trumpunafanya kabla ya Biden kuchukua urais Januari 20.
EmoticonEmoticon